Jeremiah 46:10-14


10 aLakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
siku ya kulipiza kisasi,
kisasi juu ya adui zake.
Upanga utakula hata utakapotosheka,
hadi utakapozima kiu yake kwa damu.
Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu
kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.


11 b“Panda hadi Gileadi ukapate zeri,
ee Bikira Binti wa Misri.
Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;
huwezi kupona.

12 cMataifa yatasikia juu ya aibu yako,
kilio chako kitaijaza dunia.
Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,
nao wataanguka chini pamoja.”

13 dHuu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:
14 e“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,
hubiri pia katika Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
na Tahpanhesi:
Ni mji katika Misri.

‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,
kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’
Copyright information for SwhKC